Pakua sasa Bandarini SACCOS App  ufurahie huduma zetu kupitia simu yako ya kiganjani

BANDARINI SACCOS YASHIRIKI MAADHIMISHO YA 74 YA SIKU YA KIMATAIFA YA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO (ICUD) KWA MWAKA 2022

BANDARINI SACCOS YASHIRIKI MAADHIMISHO YA 74 YA SIKU YA KIMATAIFA YA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO (ICUD) KWA MWAKA 2022

Bandarini SACCOS imeshiriki Maadhimisho ya 74 ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na Mikopo (ICUD) ambapo kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha kuanzia tarehe 16/10/2022 hadi tarehe 20/10/2022. Maadhimisho hayo yalioongozwa na kauli mbiu yaImarisha Uwezo Wako wa Kifedha Kwa Siku Zijazo Kupitia Ushirika Wa Akiba Na Mikopo”. Mgeni Rasmi wa ufunguzi wa Maadhimisho hayo alikuwa ni Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe na aliyefunga alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Adam Malima, ambapo Viongozi wote hao walipata nafasi ya kutembelea Banda la Bandarini SACCOS na kufurahishwa na ubunifu wa bidhaa zinazotolewa na Bandarini SACCOS.

Katika Maadhimisho hayo Bandarini SACCOS ilishinda kikombe cha Banda Bora katika maonyesho hayo, ambapo kikombe hicho kilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Adam Malima na kupokelewa na Mwenyekiti wa Bandarini SACCOS Bw. Ernest Nyambo.

Post a Comment

Translate »