TANGAZO LA UCHAGUZI WA NAFASI ILIYOWAZI YA MJUMBE WA BODI YA BANDARINI SACCOS LTD
Uongozi wa Bandarini SACCOS unapenda kuwatangazia wanachama wenye sifa za kugombea nafasi iliyowazi ya Mjumbe wa Bodi ya Bandarini SACCOS kuchukua fomu kuanzia tarehe 14/10/2022 hadi tarehe 21/10/2022. Fomu zitapatikana katika ofisi za Bandarini SACCOS zilizopo Jengo la Utumishi la zamani lililopo katika ofisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 14/10/2022 saa 2:00 Asubuhi na mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 21/10/2022 saa 10:00 alasiri kwa ajili ya hatua zaidi za usimamizi wa zoezi hilo la uchaguzi. Aidha, Mkutano wa Uchaguzi utafanyika tarehe 30/10/2022 katika ukumbi wa mikutano uliopo ghorofa ya 4 katika Jengo la Bandari (One stop Center).
SIFA ZA MGOMBEA NAFASI YA UONGOZI WA BANDARINI SACCOS LTD
- Awe mjumbe mwakilishi kutoka Dar es salaam Port na Makao Makuu (HQ)
- Awe na elimu ya angalau stashahada ya juu au shahada ya uhasibu na fedha, uchumi, TEHAMA, uongozi au fani nyinginezo zinazohusiana na fedha na ushirika
- Awe mwadilifu na mwaminifu
- Awe hajawahi kupoteza sifa za uongozi katika ngazi yoyote ya Chama cha Ushirika
- Awe na uwezo wa kuongoza
- Asiwe kiongozi aliyemaliza muda wake wa kisheria
- Awe anashiriki kikamilifu katika shughuli zote za Chama bila kutetereka
- Awe hajawahi kusababisha hasara katika Chama chochote cha ushirika
- Asiwe na tabia ya kulaza na kuchepusha madeni katika taasisi zingine
- Awe amethibitishwa kazini
- Awe mwanachama kwa kipindi kisichopungua miaka 3 na kuhudhuria mikutano angalau kwa miaka miwili
- Asiwe na deni alilolipata nje ya utaratibu