Pakua sasa Bandarini SACCOS App  ufurahie huduma zetu kupitia simu yako ya kiganjani

KUHUSU CHAMA CHETU

Historia Fupi

Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa Shirika la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, ulianzishwa rasmi na kusajiliwa katika Daftari la Serikali tarehe 1/8/1968 Mkoani Dar es salaam. Ushirika huu Ulisajiliwa chini ya sheria ya Vyama vya Ushirika ya Mwaka 1968. Makao Makuu yake yapo wilayani Temeke katika Jengo la Utawala Shirika la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA). Hati yake ya Usajili katika daftari la Serikai ni DRS.1861. Kufuatana na mabadiliko ya mara kwa mara ya sheria ya Vyama vya Ushirika hivi sasa Chama kinafanya kazi zake chini ya sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya Mwaka 2013 na Kanuni za SACCOS za Mwaka 2015, Sheria za Asasi ndogo za Kifedha za Mwaka 2018 na Kanuni za SACCOS za Mwaka 2019 pamoja na Masharti ya toleo la mwaka 2020. Chama hiki kilianza na wanachama 56 waliotokana na shirika la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania na hadi kufikia Mwezi Disemba 2021 Chama kilikuwa na wanachama hai 1,286.

1
2
3

DIRA

Kuwa SACCOS kiongozi inayotoa huduma na bidhaa bora za kifedha kwa Wanachama na wadau Barani Afrika.

DHAMIRA

Kutoa huduma na bidhaa endelevu za kifedha kwa wanachama na wadau kuboresha hali zao kiuchumi na kijamii.

MIIKO NA MAADILI YA UONGOZI

i.Usawa na haki ii. Ushirikiano iii. Uwazi iv. Uaminifu v. Uwajibikaji vii. Uadilifu

DHUMUNI KUU

Dhumuni kuu la Bandarini SACCOS limited kwa mujibu wa sheria Na. 6 ya Vyama vya Ushirikaya mwaka 2013 ni kuinua, kuimarisha na kuendeleza hali za kiuchumi na kijamii za wanachama wake kwa kufuata Sheria, Kanuni na taratibu za Vyama vya Ushirika. Ili kufikia Dhumuni lake kuu Bandarini SACCOS itatekeleza madhumini yake mahususi.

MALENGO MKAKATI

Chama (Bandarini SACCOS) kiweze kufikia (DIRA) yake kwa kujiwekea malengo yake ya kimkakati kuyatekeleza ili kupata matokeo;

 1. Kuongeza idadi ya wanachama wake kwa njia ya uhamasishaji.
 2. Kuhamasisha wanachama kujiwekea akiba mbalimbali
 3. Kukuza mtaji wa ukopeshaji
 4. Kuimarisha chama kwa kufanya biashara ya kifedha kufuatana na miongozo ya utoaji wa huduma ndogo za kifedha
 5. Kuboresha muundo wa utoaji huduma ili kwenda sambamba na mifumo ya Asasi ndogo za kifedha
 6. Kuwekeza kwenye mifumo ya Tekinolojia ya habari na mawasiliano kwenye shughuli zake zote
 7. Kuongeza na kuimarisha njia za Mapato ya Chama
 8. Kuanzisha na kuendeleza programu kabambe za Masoko.

MADHUMUNI MAHUSUSI

 1. Kuhamasisha wanachama kujenga tabia ya kujiwekea Akiba mara kwa mara.
 2. Kupokea na kutunza Akiba na Amana za wanachama kwa njia rahisi na salama huku ikilipa riba kwa kuzingatia soko kadri wanachama watakavyokubaliana.
 3. Kutafuta vyanzo vya fedha kujenga na kuimarisha Mtaji kwa ajili ya kutoa Mikopo kwa wanachama kwa Masharti na Riba nafuu.
 4. Kuwaelimisha wanachama kujijengea tabia ya kukopa kwa busara na kutumia vizuri mikopo yao kwa ajili ya kuinua hali zao za kiuchumi na kijamii.
 5. Kubuni na kutoa huduma na bidhaa mbalimbali za kifedha kwa wanachama waweze kushiriki zaidi katika kuimarisha Mtaji wa chama na Mitaji yao binafsi ili kuleta mvuto kwa wasio wanachama kujiunga.
 6. Kuweka kwa usalama fedha za chama na wanachama kwa kuanzisha mipango ya kukabiliana na majanga na/au kuweka bima za fedha zinazofaa.
 7. Kuwashauri wanachama kuandaa mipango yao ya maendeleo katika kuwekeza mitaji kwenye miradi ya kiuchumi na huduma za jamii yenye tija.
 8. Kutoa elimu na mafunzo mbalimbali kwa wanachama, Bodi na watendaji kuendana na kasi ya ushindani katika biashara kwenye soko la fedha.
 9. Kutoa elimu kwa wanachama kuhusu dhana ya ushirika, elimu ya Fedha na manufaa yake, ujasiriamali katika Biashara, Usindikaji na tasnia nyingine zinazohusiana na miradi inayoendeshwa na kutekelezwa na wanachama wake.
 10. Kuwekeza katika Taasisi za kifedha Hisa na Dhamana kwenye vyombo vya Fedha, Serikali na Taasisi zingine kwa manufaa ya Chama na Wanachama wake.
 11. Kufanya mambo mengine ambayo yataimarisha na kuendeleza hali ya uchumi wa chama na wanachama.
 12. Kuweka mfumo thabiti wa TEHAMA katika shughuli zote zinazoendeshwa na chama.

TAMKO LA UWEZO WA CHAMA

Chama hiki kina uwezo mkubwa kutokana na kuwa na Bodi yake ya Uongozi, Kamati zake na watendaji kuwa na sifa, weledi na uzoefu mkubwa wa kuendesha na kusiamia shughuli za uendeshaji wa ushirika wa Akiba na Mikopo. Hivyo chama kinatamka kuwa kina uwezo wa kielimu na kitaaluma unaojitosheleza kuhudumia wanachama wake katika maeneo yafuatayo;

 1. Uzoefu wa ndani ya nchi na nje katika kubuni sera mbalimbali za chama ikiwa pamoja na sera ya uhamasishaji wa wanachama kujenga tabia ya kujiwekea Akiba mara kwa mara na kuzitunza fedha hizo mahali salama.
 2. Kuwa na uzoefu na taaluma ya kutosha katika utafutaji wa mitaji ya kibiashara na ile ya kutoa mazao ya kifedha iyanayoshabihiana na mahitaji yao Msingi na vipaumbele vyao kwa gharama nafuu na kasi inayohitajika.
 3. Chama kina uwezo unaojitosheleza katika kubuni Mitaala ya Kimafunzo inayohitaji kutambua haki na wajibu wao, elimu za kibiashara na uweezaji, masuala ya kifedha, ujasiriamali, ushirika na Usindikaji.
 4. Chama kina uwezo wa kulinda Mali na fedha za Chama kwa kuweka kinga za Matengo pamoja na Bima mbalimbali za fidia kutokana na Mali za Chama zitakazokuwa zinaharibika
 5. Uwezo na uzoefu mkubwa wa kuhudumia wanachama katika kuwasikiliza hoja na kero zao, na kuzipatia ufumbuzi, kuwapatia mahitaji ya mazao ya chama kufuatana na mahitaji yao.
 6. Chama kina uwezo na uzoefu wa muda mrefu wa kutunza kumbukumbu zao mbalimbali pindi wakihitaji kuziona wakati wowote wanazipata.
 7. Chama kina uwezo mkubwa na uzoefu wa kutosha katika kuandaa taarifa na kuzifikisha kwao kwa wakati ili kutathmini na kutambua fedha zao ziko wapi na zinaafanya nini.
 8. Chama kina uwezo na taaluma ya kutosha ya uwekezaji wenye tija ambao unalenga mahitaji ya pamoja ya wanachama wote.
Translate »