UANACHAMA
Kwa mujibu wa Msingi wa kwanza (1) wa Ushirika kimataifa na Masharti ya chama ibara ya 10, Uanachama wa Bandarini SACCOS uko wazi kwa mtumishi yeyote yule wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Taasisi ya umma au binafsi ili mradi tu awe tayari kufaidika na huduma zake na kufuata Sheria, Kanuni, na Masharti ya Bandarini SACCOS limited. Wanachama ni wale wote waliokuwepo tokea kuanzishwa kwake na wanaoendelea kujiunga kwa mujibu wa masharti ya Chama
- Uwe mwajiriwa wa Taasisi ya umma au binafsi
- Kujaza fomu ya uanachama
- Kulipa kiingilio cha Sh. 100,000
- Kuchangia akiba ya 7% ya kipato chako kila mwezi
- Kulipa hisa kila mwezi (kima cha chini Sh. 10,000)
- Kuchangia michango ya mwezi kupitia mshahara
- Kuitambulisha Bandarini SACCOS Ltd kwa mwajiri
- Huduma zingine zitatolewa kwa kuzingatia vigezo na masharti ya huduma husika.
Katika ubunifu wa mazao ya bidhaa za kifedha na Huduma kwa wanachama na wadau wa Bandarini SACCOS wanafaidika na;
- Viwango vya riba vya mikopo ambavyo ni shindani na nafuu.
- Mapato ya kuvutia kwa wanachama wanaowekeza fedha zao kupitia Akiba, Amana, na Akiba Maalum.
- Uchaguzi mpana wa bidhaa za kifedha, hususan mikopo.
- Uwazi wa gharama katika miamala ya uchukuaji wa Amana na Akiba Maalum.
- Malipo ya gawio kwa wanahisa pamoja na riba kwenye Akiba na Amana.
- Ulinzi dhidi ya majanga yanayoweza kuathiri mikopo.
- Nafasi ya kushiriki majadiliano kuhusu uwekezaji wa fedha zao.
- Kukamilisha kununua hisa na kuweka akiba kwa kuzingatia
Masharti sera na miongozo iliyopo katika chama. - Kufuata na kutekeleza Sera, Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama, maazimio ya
Mikutano mikuu na maelekezo mengine halali kwa mujibu wa Sheria za nchi; - Kurejesha mkopo kwa kufuata mkataba wa mkopo;
- Kutoa michango mbalimbali katika kuendeleza madhumuni ya chama kadri itakavyoamuliwa na Mkutano Mkuu;
- Kubeba dhamana endapo janga lolote litakipata chama;
- Kuwa mwaminifu na kuonesha ushirikiano katika kutekeleza shughuli za chama;
- Kumdhamini mkopo mwanachama mwenzake isipokuwa mwanachama aliyedhamini hatakuwa na haki yakudhaminiwa na mwanachama aliyemdhamini katika kipindi kile kile;
- Kuhudhuria semina na mafunzo yanayotolewa na Bandarini SACCOS katika mpango wake wa elimu na mafunzo mengine yatakayotolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika au wadau wa kisekta.
- Kushiriki kikamilifu katika shughuli za Chama ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mikutano yote inayohusika;
- Kushiriki katika kutoa uamuzi wa mambo mbalimbali katika Mikutano Mikuu;
- Kupiga kura chini ya misingi ya mtu mmoja kura moja bila kujali idadi ya Hisa anazomiliki;
- Kuchagua na/au kuchaguliwa katika Uongozi wa chama.
- Kuwa na haki sawa kuhusu mali ya Chama na kudhibiti ipasavyo matumizi yake;
- Kupatiwa huduma zozote zinazotolewa na chama ilimradi amekidhi masharti yanayoambatana na huduma hiyo;
- Kupatiwa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za Bandarini SACCOS, muhtasari wa mkutano na nyaraka nyingine za chama kwa ajili ya mapitio akiwa katika ofisi za chama;
- Kuteua Mrithi;
- Kupokea gawio na faida nyingine kutoka katika shughuli za chama kwa kuzingatia masharti; na
- Kupewa kitabu cha Akiba au kifaa kingine chenye makusudi hayo.