TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA 54 UTAKAOFANYIKA TAREHE 30 OKTOBA 2022
Bodi ya Uongozi inawatangazia wanachama wote ambao ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama,kwamba Mkutano Mkuu wa 54 kwa Mwaka 2022 utafanyika Dar es salaam tarehe 30 Oktoba 2022 katika ukumbi wa mikutano uliopo Jengo la Bandari (One stop Centre) ghorofa ya nne, jijini Dar es salaam kuanzia saa 02:00 asubuhi.
ZIFUATAZO NI AGENDA ZA MKUTANO MKUU WA 54:
- Kufungua Mkutano
- Kuthibitisha akidi
- Kuchagua Mwenyekiti wa Mkutano
- Kupokea na kuthibitisha agenda za Mkutano
- Kusoma na kuthibitisha Muhtasari wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa 53
- Yatokanayo na Muhtasari wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa 53
- Kupokea na kuthibitisha wanachama wapya na wanaotoka
- Kupokea Taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi
- Kupokea Taarifa ya Kamati ya Usimamizi
- Kupokea na kuthibitisha Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za mwaka 2021
- Kupokea na kuthibitisha Makisio ya Mapato na Matumizi ya mwaka 2023
- Uchaguzi wa nafasi wazi ya Mjumbe wa Bodi
- Mengineyo
- Kufunga Mkutano
Ninawatakia wajumbe wote maandalizi mema na ushiriki mzuri wa Mkutano huo pamoja na mwisho wa mwaka wenye Amani.