Pakua sasa Bandarini SACCOS App  ufurahie huduma zetu kupitia simu yako ya kiganjani

MIKUTANO YA MATAWI KWA 2022 YAANZIA MKOANI MTWARA

MIKUTANO YA MATAWI KWA 2022 YAANZIA MKOANI MTWARA

Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa mwaka wa chama huanza kwa kufanya mikutano ya matawi katika vituo mbalimbali waliopo wanachama ikiwa na lengo la kutoa mrejesho wa utekelezaji wa maazimio ya Mkutano Mkuu wa Chama wa mwaka uliopita na kukusanya ndondoo za wanachama pamoja na kujibu hoja mbalimbali za wanachama ili kuwapa uelewa wanachama namna chama chao kinavyooendeshwa.

Kwa mwaka 2022 mikutano ya matawi imeanzia Mkoani Mtwara ambapo wanachama wa Bandarini SACCOS waliopo katika Bandari ya Mtwara walipewa mrejesho wa utekelezaji wa maazimio ya Mkutano Mkuu wa 53 uliofanyika mwaka 2021, kutoa maoni na hoja mbalimbali pamoja na kufanya uchaguzi wa Mjumbe mwakilishi wa wanachama. Mkutano huo wa wanachama ulifanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Bandari ya Mtwara ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni ndugu James Ng’wandu ambae alimuwakilisha Meneja wa Bandari ya Mtwara pamoja na Mrajis Msidizi wa mkoa wa Mtwara Ndugu Hamidu Ndago.

Post a Comment

Translate »