ATHUMAN KOSHUMA MWAKILISHI MPYA WA WANACHAMA BANDARI YA MTWARA
Katika Mkutano wa wanachama wa Bandari ya Mtwara uliofanyika tarehe 20/05/2022 kulikuwa na agenda ya Uchaguzi wa Mwakilishi wa wanachama kwa ajili ya kuongeza muwakilishi mmoja kutokana na idadi ya wanachama waliopo katika Bandari ya Mtwara kufikia zaidi 100 ambapo idadi ya wawakilishi waliopo awali haendani na idadi hiyo ya wanachama, ambapo awali Bandari ya Mtwara ilikuwa inawawakilishi 4 na kwa mujibu wa masharti na miongozo ya Bandarini SACCOS muwakilishi mmoja huwakilisha wanachama 20.
Uchaguzi ulifanyika chini ya usimamizi wa Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Mtwara Ndugu Hamidu Ndago, ambapo katika uchaguzi huo alijitokeza mgombea mmoja pekee Ndugu Athuman Koshuma aliyepita kwa kupigiwa kura za ndio na wanachama wote waliokuwepo katika Mkutano. Hivyo kufanya idadi ya wawakilishi wa wanachama katika tawi la Bandari ya Mtwara kufikia wawakilishi 5, ambao ni;
- Khalfan Abdallah Genge
- Theresia Mangwinda John
- Rehema Raymond Jomal
- Baraka Mwakalibure Edwin
- Athumani Rajab Koshuma