WANACHAMA MTWARA WAPEWA VYETI VYA UMILIKI WA HISA
Katika Mkutano wa wanachama uliofanyika katika Bandari ya Mtwara tarehe 20/05/2022, wanachama waliomaliza kununua Hisa kwa mujibu wa miongozo na masharti ya chama ambazo ni Hisa 50 zenye thamani ya Tsh. 500,000.00 walikabidhiwa vyeti vya umiliki wa Hisa (share certificate), ambapo vyeti hivyo vilitolewa na Mgeni Rasmi Ndugu James Ng’wandu aliyemuwakilisha Meneja wa Bandari ya Mtwara.