Pakua sasa Bandarini SACCOS App  ufurahie huduma zetu kupitia simu yako ya kiganjani

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI – AFISA TEHAMA, AFISA MIKOPO NA MSARUFI (TELLER)

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI – AFISA TEHAMA, AFISA MIKOPO NA MSARUFI (TELLER)

Bandarini SACCOS LTD ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo kinachotoa huduma ndogo za kifedha kwa wanachama wake. Chama kinatangaza nafasi tatu (3) wazi za Afisa Tehama, Afisa Mikopo na Msarufi (Teller) kwa watanzania wenye sifa kama zilivyoainishwa hapa chini.

1. AFISA TEHAMA (1)

Atakuwa msaidizi mkuu wa Afisa Tehama Mkuu katika kuhakikisha wakati wote kunakuwa na mfumo wa upashanaji habari uliothabiti, ulinzi na kutumika ndani ya Bandarini SACCOS lakini pia unaojitosheleza kulingana na mahitaji ya chama.

SIFA ZA AFISA TEHAMA
 1. Awe na elimu isiyopungua Shahada ya kwanza katika fani za Sayansi ya Computer au/na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano au inayolingana na hizo kutoka chuo kinachotambulika na Serikali,
 2. Awe na ujuzi wa ziada katika masuala ya teknolojia yafuatayo (Oracle, PHP/MySQL, React Js/ Node Js/ Redux, Javascript, JQuery, CSS, Linux OS, REST/ SOAP, XML, JSON, na Ms   SQL Server),
 3. Awe na uwezo wa kutumia mifumo ya Co-Banking System na mifumo mingine ya TEHAMA,
 4. Awe na umri usiozidi miaka 35,
 5. Awe na uzoefu usiopungua mwaka mmoja (1) kwa kazi husika,
 6. Awe tayari kufanya kazi katika usimamizi duni, na
 7. Mwenye uelewa na masuala ya mifumo katika uendeshaji wa SACCOS atapewa kipaumbele.
2. AFISA MIKOPO (1)

Atawajibika kwa Afisa Mikopo Mkuu kwa masuala yote yanayohusu uwekaji akiba, uombaji, uchambuzi, utoaji, urejeshaji na ufuatiliaji wa mikopo yote itakayotolewa na Bandarini SACCOS.

SIFA ZA AFISA MIKOPO
 1. Awe na elimu ya Shahada ya kwanza ya Usimamizi wa Ushirika na Uhasibu, Shahada ya Uhasibu au fani inayofanana na hizo kutoka katika chuo kinachotambulika na Serikali,
 2. Awe na uzoefu wa kufanya kazi katika taasisi ya fedha kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja (1),
 3. Awe na uelewa mkubwa katika masuala ya Mikopo kwenye SACCOS,
 4. Awe na ujuzi wa matumizi ya Computer hususan mifumo ya uhasibu,
 5. Awe na umri usiozidi miaka 35,
 6. Awe tayari kufanya kazi katika usimamizi duni.
 7. Mwenye Shahada ya Ushirika; na/au Shahada ya Uhasibu, fedha na uzoefu katika masuala ya SACCOS atapewa kipaumbele.
3. MSARUFI (TELLER) (1)

Atafanya kazi kwenye huduma za mbele (front office) au kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi na atawajibika kwa Mhasibu wa Bandarini SACCOS.

SIFA ZA MSARUFI (TELLER)
 1. Awe na elimu ya Stashahada ya Usimamizi wa Ushirika, Uhasibu, Fedha au/na fani inayofanana na hizo kutoka katika chuo kinachotambulika na Serikali,
 2. Awe na uelewa wa matumizi ya komputa hususan mifumo ya uhasibu,
 3. Awe na umri usiozidi miaka 35,
 4. Awe tayari kufanya kazi katika usimamizi duni, na
 5. Mwenye Stashahada ya Ushirika; na/au Stashahada ya Uhasibu, fedha na uzoefu katika masuala ya SACCOS atapewa kipaumbele
VIAMBATANISHO
 • Barua ya maombi ya kazi,
 • Wasifu wa muombaji (CV),
 • Nakala za vyeti vya taaluma na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali,
 • Nakala ya cheti cha kuzaliwa,
 • Nakala ya kitambulisho cha taifa/kupiga kura/leseni ya udereva/pasi ya kusafiria /barua ya utambulisho wa makazi kutoka serikali za mitaa,
 • Nakala zote ziwasilishwe pekee zilizothibitishwa na Mwanasheria anayetambulika na Serikali au/na Kamishna wa Viapo, na
 • Kwa waombaji walioko makazini waambatishe rejea ya uthibitisho kutoka taasisi anayotoka.
MASLAHI KWA ATAKAEPITISHWA

Mshahara mnono na Marupurupu mazuri kulingana na ngazi za mshahara kama zilivyo katika Kanuni za Ajira na Utumishi za Bandarini SACCOS vitatolewa kwa atakaepitishwa na kuajiriwa kwa nafasi husika.

KIPINDI CHA KUPOKEA MAOMBI

Maombi yatapokelewa kuanzia tarehe ya tangazo hili hadi tarehe 12 Juni 2022 saa 10:00 jioni.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI

Maombi yote kwa nafasi tajwa hapo juu yawasilishwe kwa mkono katika ofisi za Bandarini SACCOS LTD zilizopo katika Jengo la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari ghorofa ya 3 (Utumishi ya zamani) Kilwa road, Dar es Salaam, Tanzania na yaelekezwe kwa anuani ifuatayo:-

Meneja,

Bandarini SACCOS LTD,

S.L.P. 50091,

DAR ES SALAAM

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA
BODI YA UONGOZI WA BANDARINI SACCOS LTD

Post a Comment

Translate »