Pakua sasa Bandarini SACCOS App  ufurahie huduma zetu kupitia simu yako ya kiganjani

BANDARINI SACCOS YAZINDUA HUDUMA YA MBALIMBALI ZA MIKOPO

BANDARINI SACCOS YAZINDUA HUDUMA YA MBALIMBALI ZA MIKOPO

Katika Mkutano Mkuu wa 54 wa mwaka 2022 Bandarini SACCOS imezindua huduma zifuatazo ambazo zinalenga kuboresha utoaji wa huduma kwa wanachama;

1. HUDUMA YA UWAKALA WA BIMA

Huduma ya uwakala wa bima kutoa bima kwa wanachama na wasiowanachama wa Bandarini SACCOS kwa gharama nafuu na uharaka katika kushughulika madai pindi janga linapotokea. Kwa wanachama watakaokata bima kupitia Bandarini SACCOS wataweza kunufaika na mkopo wa Jikinge unaomuwezesha mwanachama asiyeweza kumudu gharama za bima kunufaika na huduma ya bima huku akikatwa kidogo kidogo kupitia mkopo wa jikinge.

2. MKOPO WA SAFARI

Mkopo huu ni maalum kwa wanachama wanahitaji kusafiri maeneo mbalimbali kwa malengo ya Kibiashara, kujifunza, starehe na kidini kama vile Makka na Israel. Kupitia Mkopo huu Bandarini SACCOS kwa kushirikiana na Firstfly Safari itakulipia gharama zote za safari yako ambapo utakuwa ukirejesha mkopo huo kidogo kidogo kwa muda wa hadi miezi 36.

3. MKOPO WA VIFAA VYA ELETRONIKI KUTOKA DUKANI KWETU

Mkopo huu unamuwezesha mwanachama wa Bandarini SACCOS kumudu gharama za manunuzi ya vifaa mbalimbali vya kieletroniki kutoka Dukani Kwetu ambavyo ni halisi (original) na vina warranty ya muda mrefu lakini pia usafiri na ufungwaji wa kifaa ni bure, na mwanachama atalipa kidogo kidogo kifaa hicho kwa muda wa hadi miezi 36.

4. MKOPO WA VIFAA VYA NYUMBANI KUTOKA VON HOTPOINT

Mkopo huu unamuwezesha mwanachama wa Bandarini SACCOS kumudu gharama za manunuzi ya vifaa mbalimbali vya nyumbani kutoka Von Hotpoint ambavyo ni halisi (original) na vina warranty ya muda mrefu, na mwanachama atalipa kidogo kidogo kifaa hicho kwa muda wa hadi miezi 36.

5. MKOPO WA VING’AMUZI NA VIFURUSHI KUTOKA DSTV

Mkopo huu unamuwezesha mwanachama wa Bandarini SACCOS kumudu gharama za manunuzi ya ving’amuzi na vifurushi vya DSTV vya mwaka mzima, ambapo mwanachama atalipa kidogo kidogo kwa muda wa hadi miezi 12.

Post a Comment

Translate »