BANDARINI SACCOS YATOA MSAADA SHULE YA MSINGI YA WATOTO WENYE ULEMAVU WAILES ILIYOPO TEMEKE
Leo tarehe 24/10/2022 Bandarini SACCOS imetoa msaada wa vifaa saidizi vya kufundishia pamoja na vyakula katika Shule ya Msingi ya Watoto wenye ya Temeke Wailes, ikiwa ni katika Maadhimisho ya wiki ya Bandarini SACCOS ambapo Bandarini SACCOS hufanya matukio mbalimbali ya kujali jamii. Msaada huo ulipokelewa na Mkuu wa Shule hiyo Bw. Barakaeli Kanuya.