Pakua sasa Bandarini SACCOS App  ufurahie huduma zetu kupitia simu yako ya kiganjani

BANDARINI SACCOS YATOA MSAADA WA KADI 150 ZA BIMA ZA AFYA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM.

BANDARINI SACCOS YATOA MSAADA WA KADI 150 ZA BIMA ZA AFYA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM.

Leo tarehe 28 Oktoba 2022 Bandarini SACCOS imetoa msaada wa kadi 150 za Bima ya afya kwa watoto wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu na Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu katika kata ya kurasini, Ambapo kadi hizi zilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh. Joketi Mwegelo pamoja na Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa Ya Temeke Mh. Arnold Sangawe.

Pia siku hii iliambatana na zoezi la kuwatembeza watoto wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu katika maeneo ya Bandari ya Dar es Salaam Ikiwa ni sehemu ya kujifunza na kuona shughuli mbalimbali katika Bandari ya Dar es Salaam.

Post a Comment

Translate »