BANDARINI SACCOS YATOA MSAADA WA VIFAA VYA USAFI KATIKA GEREZA LA KEKO DAR ES SALAAM,
Tarehe 27 Oktoba 2022 Bandarini SACCOS ikiongozwa na wajumbe wa Bodi pamoja na menejimenti imefanikiwa kutoa msaada wa vifaa vya usafi katika Gereza la Keko Lililopo Temeke Dar es salaam, Tukio hili likiwa ni muendelezo wa kusaidia jamii katika maadhimisho ya wiki ya Bandarini SACCOS kwa mwaka 2022.