KIKAO CHA MAKABIDHIANO YA MRADI WA UJENZI WA OFISI YA BANDARINI SACCOS
Leo tarehe 23/09/2022 Bandarini SACCOS imeshiriki katika kikao cha makabidhiano ya mradi wa Jengo la Ofisi ambapo mradi huo ulikuwa ukisimamiwa na kampuni ya Ujenzi ya SUMA JKT. Mgeni rasmi katika kikao hicho alikuwa ni Bw. Mrisho S. Mrisho ambae ni Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es salaam.
Pia makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Bi. Olivia Kaiza ambaye alimuwakilisha Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Dar es salaam, Bw. Baraka Mwakamela ambae ni Afisa Ushirika Manispaa ya Temeke, Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT Eng. Morgan Nyonyi, Meneja wa mradi, Viongozi wa Bandarini SACCOS pamoja na watendaji wa Bandarini SACCOS na SUMA JKT.