Pakua sasa Bandarini SACCOS App  ufurahie huduma zetu kupitia simu yako ya kiganjani

SEMINA NA MKUTANO KWA WANACHAMA WA KIGOMA

SEMINA NA MKUTANO KWA WANACHAMA WA KIGOMA

Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa mwaka wa chama huanza kwa kufanya Semina na Mikutano ya matawi katika vituo mbalimbali waliopo wanachama ikiwa na lengo la kutoa mrejesho wa utekelezaji wa maazimio ya Mkutano Mkuu wa Chama wa mwaka uliopita na kukusanya ndondoo za wanachama pamoja na kujibu hoja mbalimbali za wanachama ili kuwapa uelewa wanachama namna chama chao kinavyooendeshwa.

Tarehe 12/06/2022 wanachama wa Bandarini SACCOS kituo cha Bandari ya Kigoma walipewa semina kuhusu elimu ya fedha na ushirika ikiwa ni katika kuwajengea uwezo wanachama katika kuufahamu ushirika kwa undani na pia kuwa na elimu ya fedha itakayowasaidia katika kufikia malengo yao ya muda mrefu na muda mfupi. Pia walifanya Mkutano ambapo pamoja na mengine mengi, walipewa mrejesho wa utekelezaji wa maazimio ya Mkutano Mkuu wa 53 uliofanyika mwaka 2021 pamoja na kutoa maoni mbalimbali kwa ajili ya ustawi wa Bandarini SACCOS. Mkutano huo wa wanachama ulifanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Bandari ya Kigoma ambapo Mwenyekiti wa Bandarini SACCOS Bw. Ernest Nyambo alikabidhi Vyeti vya umiliki wa Hisa kwa wanachama waliokamilisha ununuzi wa Hisa 50 zenye thamani ya Tsh. 500,000.

Post a Comment

Translate »