Bandarini SACCOS Ltd inawahamasisha wanachama wake kushiriki kikamilifu katika mpango wa uchangiaji wa akiba ili kujenga msingi imara wa kifedha. Uchangiaji wa akiba ni muhimu kwa maendeleo ya wanachama na ustawi wa chama kwa ujumla. Kila mwanachama wa Bandarini SACCOS anatakiwa kuchangia 7% ya kipato chake cha msingi (basic salary) kila mwezi.





Faida za kuweka
Akiba
Kukuza Mtaji wa Kibinafsi - Akiba yako hukua kila mwezi na itakusaidia kufanikisha malengo yako ya kifedha.
Kuongeza uwezo wa Kukopesheka – Mwanachama wa Bandarini SACCOS Ltd atakopa mara ya tano ya akiba yake.
Usalama wa Kifedha – Akiba ni kinga ya dharura na husaidia kujenga utamaduni wa matumizi endelevu.
Kukuza Uwezo wa Kifedha - Akiba hujenga nidhamu ya kifedha na kuwezesha mipango endelevu ya kiuchumi.
Ribaa juu ya akiba - Bandarini SACCOS Ltd inatoa faida ya 4% kila mwaka kwenye akiba za wanachama