Pakua sasa Bandarini SACCOS App  ufurahie huduma zetu kupitia simu yako ya kiganjani

Image Alt

Hisa

Hisa ni sehemu ya umiliki wa Bandarini SACCOS Ltd na wanachama wote wanahitajika kumiliki hisa ili kuwa na haki ya kupata huduma mbalimbali za Chama pamoja na kupata gawio kutokana kwa faida inayozalishwa.

Thamani ya Hisa

Kila hisa moja ina thamani ya shilingi elfu kumi (10,000). Hii inamaanisha kwa kila hisa moja unayonunua, utalipa shilingi 10,000.

Ukomo wa umiliki wa Hisa

Hisa za uanachama Bandarini SACCOS Ltd hazina kikomo, yaani, wanachama wataendelea kununua hisa kila mwezi kwa kima cha chini cha shilingi 10,000 katika kipindi chote cha uanachama.

Kima cha Chini cha Umiliki wa Hisa

Kila mwanachama anatakiwa kumiliki angalau hisa 50, ambazo zina jumla ya thamani ya shilingi 500,000 (50 x 10,000). Hii ni kima cha chini cha kumiliki hisa ambacho kitakuwezesha kukamilisha uanachama wako na kukuwezesha kupata huduma mbalimbali za Chama.

Gawio (Dividends)

Wanachama wote wanaomiliki hisa watakuwa wakipokea gawio kulingana na faida inayopatikana katika mwaka husika na maazimio ya Mkutano Mkuu. Gawio hili linatolewa kulingana na idadi ya hisa alizonazo mwanachama.

Translate »