Bandarini SACCOS Insurance Agency ni wakala wa bima ulioanzishwa kwa madhumuni ya kuwapatia wanachama na wateja wa Bandarini SACCOS Ltd huduma bora za bima kwa gharama nafuu. Kama sehemu ya Bandarini SACCOS Ltd, wakala huu unatoa huduma za bima kwa kuzingatia mahitaji ya kifedha ya wanachama wake, huku ukihakikisha ulinzi wa mali na ustawi wao wa kifedha.
Bandarini SACCOS Insurance Agency inashirikiana na makampuni makubwa ya bima ili kuwapatia wanachama wake huduma bora katika aina mbalimbali za bima, zikiwemo bima za vyombo vya usafiri, bima ya jengo, biashara n.k
FAIDA ZA KUCHAGUA BANDAINI SACCOS INSURANCE AGENCY
Gharama Nafuu
Gharama nafuu na Mkopo kwa wanachama wa Bandarini SACCOS Ltd
Ushauri wa kitaalamu
Ushauri wa kitaalamu kuhusu aina bora ya bima kulingana na mahitaji yako.
Uharaka wa Madai ya Bima
Huduma za haraka na rahisi za madai ya bima.
Uhakika wa Huduma
Ushirikiano na kampuni za bima zinazoaminika.
WATAALAMU WETU WA BIMA WAPO TAYARI KUKUHUDUMIA
Bandarini SACCOS Insurance Agency, tuna timu ya wataalamu wa bima waliobobea katika sekta hii, wenye uzoefu na uelewa wa kina kuhusu huduma mbalimbali za bima. Lengo letu ni kuhakikisha wanachama wetu na wateja wanapata huduma bora, ushauri sahihi, na suluhisho la bima linalokidhi mahitaji yao.

PRINCIPAL
ISMAIL H. ISMAIL

AFISA BIMA
GLADNESS KILIMO
HUDUMA ZETU
Bandarini SACCOS Insurance Agency inatoa huduma mbalimbali za bima za mali na biashara (General Insurance) ili kuwapa wanachama na wateja wake ulinzi wa kifedha dhidi ya majanga yasiyotarajiwa. Tunashirikiana na makampuni ya bima yanayoaminika kuhakikisha unapata huduma bora kwa gharama nafuu.