Pakua sasa Bandarini SACCOS App  ufurahie huduma zetu kupitia simu yako ya kiganjani

TANGAZO LA UCHAGUZI WA WAWAKILISHI

TANGAZO LA UCHAGUZI WA WAWAKILISHI

TANGAZO LA UCHAGUZI WA WAWAKILISHI WA WANACHAMA WA BANDARINI SACCOS LTD

Uongozi wa Bandarini SACCOS unapenda kuwatangazia wanachama wenye sifa za kugombea nafasi ya Uwakilishi wa Wanachama wa Bandarini SACCOS LTD katika Vituo mbali mbali kuchukua fomu kuanzia tarehe 14/05/2026 hadi tarehe 20/05/2026 Fomu zitapatikana katika ofisi za Bandarini SACCOS zilizopo Mkabala na Uwanja wa Benjamin Mkapa, Temeke, Dar es Salaam kuanzia tarehe 14/05/2026 saa 2:00 Asubuhi na mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 26/05/2026 saa 10:00 alasiri kwa ajili ya hatua zaidi za usimamizi wa zoezi hilo la uchaguzi. Aidha, tarehe, muda na mahali pa Mkutano wa Uchaguzi utazingatia Ratiba ya Mikutano ya Matawi.

SIFA ZA MGOMBEA NAFASI YA UWAKILISHI WA WANACHAMA

  1. Awe na elimu ya angalau shahada au stashahada ya juu ya uhasibu na fedha, uchumi, TEHAMA, uongozi au fani nyinginezo zinazohusiana na Usimamizi wa biashara, fedha na ushirika
  2. Awe mwadilifu na mwaminifu
  3. Awe hajawahi kupoteza sifa za uongozi katika ngazi yoyote ya Chama cha Ushirika
  4. Awe na maono na uwezo wa kufanya maamuzi
  5. Awe anashiriki kikamilifu katika shughuli zote za Chama bila kutetereka
  6. Awe hajawahi kusababisha hasara katika Chama chochote cha ushirika
  7. Asiwe na tabia ya kulaza na kuchepusha madeni katika taasisi zingine
  8. Awe amethibitishwa kazini
  9. Awe mwanachama kwa kipindi kisichopungua miaka 3 na kuhudhuria mikutano ya uanachama angalau 2
  10. Asiwe na deni alilolipata nje ya utaratibu

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA UONGOZI WA BANDARINI SACCOS LTD

Post a Comment

Translate »