BANDARINI SACCOS YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TEMEKE
Leo tarehe 24 Oktoba 2022 Bandarini SACCOS imetoa msaada wa vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, ikiwa ni muendelezo wa matukio mbalimbali ya kujali jamii kwenye maadhimisho ya wiki ya Bandarini SACCOS kwa mwaka 2022. Ambapo msaada huo ulipokelewa na Mganga Mkuu wa Hospitali Dkt. Joseph Kimaro.
