Pakua sasa Bandarini SACCOS App  ufurahie huduma zetu kupitia simu yako ya kiganjani

Frequent Asked Questions (FQA)

MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA

1. Je mtu akishajiunga na chama itachukua muda gani kupata mkopo?

Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Mwanachama mpya atapata stahili ya kuomba mkopo mara baada ya kulipa kiingilio, kukamilisha angalau nusu ya Hisa za lazima na ameshaanza kukatwa michango ya akiba ya kila mwezi kutoka kwenye mshahara wake angalau kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu.

2. Naomba kujua mwanachama akiomba mkopo inachukua muda gani kukamilika kwenye Akaunti?

Mikopo midogo hulipwa ndani ya masaa 24. Mikopo mikubwa hulipwa ndani ya siku 30, au siku 7 kama vigezo vyote vimekamilika. Mwanachama anapaswa kuhakikisha amekamilisha ofa na mikataba ya mkopo.

3. Je naweza kukopa hata bila kuwa na michango?

Ndiyo, lakini tu kwa mikopo ya Papo kwa Papo na Dharura. Mikopo mikubwa lazima mwanachama awe na akiba ya kutosha (maradufu mara 5 ya akiba).

4. Naweza kufanya Top up? Kama ndio, ni kiasi gani?

Inaruhusiwa baada ya kulipa mkopo wa awali kwa miezi sita mfululizo bila kukosa.

5. Je naweza kupunguza/kuchukua sehemu ya akiba zangu?

Akiba za lazima haziwezi kurejeshwa hadi uanachama ukome. Akiba za hiari zinaweza kurejeshwa kulingana na sera.

6. Naomba kupewa utaratibu wa kupata mkopo?

1. Lazima uwe mwanachama hai. 2. Jaza fomu ya mkopo. 3. Wasilisha fomu. 4. Saini ofa na mkataba baada ya kuidhinishwa.

7. Je naruhusiwa kupunguza deni?

Ndiyo. Andika barua ya kusudio, lipa benki, wasilisha hati ya malipo na utapunguziwa deni.

8. Je naweza kulipa mkopo wote kwa mkupuo?

Ndiyo. Fuata utaratibu wa barua ya kusudio, pokea hesabu ya deni, lipa benki, na wasilisha stakabadhi ya malipo.

9. Naomba kujua taratibu za kununua madeni ya taasisi nyingine?

Wasiliana na ofisi ya SACCOS, leta uthibitisho wa deni, baada ya makubaliano SACCOS italipa na utapewa hati ya malipo.

10. Je naweza kukopa kutokana na mapato mengine nje ya mshahara?

Ndiyo, lakini marejesho hufanyika kupitia mshahara na akiba ya amana lazima iwe imefanya kazi angalau miezi mitatu.

11. Je, ukiweka akiba SACCOS inachukua muda gani kuomba mkopo?

Lazima uwe umelipa kiingilio, 50% ya hisa na akiba ya angalau mwezi mmoja.

12. Kwa nini riba ya akiba hailipwi mapema?

Riba hulipwa baada ya hesabu za robo mwaka, kulingana na sera ya uhamasishaji.

13. Kwa nini ninatakiwa kuwa na wadhamini wa mkopo wakati kuna bima?

Wadhamini ni hitaji la kisheria. Bima hulinda dhidi ya kifo au ulemavu wa kudumu. Kwa sababu nyingine, mdhamini hulipa deni.

Translate »