Pakua sasa Bandarini SACCOS App  ufurahie huduma zetu kupitia simu yako ya kiganjani

Kata Bima ya Jengo Leo Inalinda nyumba na mali nyingine dhidi ya majanga kama moto, wizi, mafuriko, au majanga mengine 01 Karibu Ukate Bima ya Gari Leo Bima hii inalinda wamiliki wa magari dhidi ya hasara kutokana na ajali, wizi, moto, au uharibifu mwingine 02 Kata Bima ya Jengo Leo Inalinda nyumba na mali nyingine dhidi ya majanga kama moto, wizi, mafuriko, au majanga mengine 03
KARIBU

BANDARINI SACCOS INSURANCE AGENCY

Bandarini SACCOS Insurance Agency ni wakala wa bima ulioanzishwa kwa madhumuni ya kuwapatia wanachama na wateja wa Bandarini SACCOS Ltd huduma bora za bima kwa gharama nafuu. Kama sehemu ya Bandarini SACCOS Ltd, wakala huu unatoa huduma za bima kwa kuzingatia mahitaji ya kifedha ya wanachama wake, huku ukihakikisha ulinzi wa mali na ustawi wao wa kifedha.

Bandarini SACCOS Insurance Agency inashirikiana na makampuni makubwa ya bima ili kuwapatia wanachama wake huduma bora katika aina mbalimbali za bima, zikiwemo bima za vyombo vya usafiri, bima ya jengo, biashara n.k

FAIDA ZA KUCHAGUA BANDAINI SACCOS INSURANCE AGENCY

1
2
3
4

Gharama Nafuu

Gharama nafuu na Mkopo kwa wanachama wa Bandarini SACCOS Ltd

Ushauri wa kitaalamu

Ushauri wa kitaalamu kuhusu aina bora ya bima kulingana na mahitaji yako.

Uharaka wa Madai ya Bima

Huduma za haraka na rahisi za madai ya bima.

Uhakika wa Huduma

Ushirikiano na kampuni za bima zinazoaminika.

WATAALAMU WETU WA BIMA WAPO TAYARI KUKUHUDUMIA

Bandarini SACCOS Insurance Agency, tuna timu ya wataalamu wa bima waliobobea katika sekta hii, wenye uzoefu na uelewa wa kina kuhusu huduma mbalimbali za bima. Lengo letu ni kuhakikisha wanachama wetu na wateja wanapata huduma bora, ushauri sahihi, na suluhisho la bima linalokidhi mahitaji yao.

PRINCIPAL
ISMAIL H. ISMAIL
AFISA BIMA
GLADNESS KILIMO

HUDUMA ZETU

Bandarini SACCOS Insurance Agency inatoa huduma mbalimbali za bima za mali na biashara (General Insurance) ili kuwapa wanachama na wateja wake ulinzi wa kifedha dhidi ya majanga yasiyotarajiwa. Tunashirikiana na makampuni ya bima yanayoaminika kuhakikisha unapata huduma bora kwa gharama nafuu.

Bima ya Magari (Motor Insurance)

Bima hii inalinda wamiliki wa magari dhidi ya hasara kutokana na ajali, wizi, moto, au uharibifu mwingine. Tunatoa aina mbili za bima ya gari, Bima kubwa (Comprehensive Insurance ) na Bima Ndogo (Third Party Insurance).

Bima ya Nyumba na Mali (Home & Property Insurance)

Inalinda nyumba na mali nyingine dhidi ya majanga kama moto, wizi, mafuriko, au majanga mengine. Bima hii ni muhimu kwa wamiliki wa nyumba na wamiliki wa biashara.

Bima ya Usafirishaji wa Mizigo (Marine & Cargo Insurance)

Husaidia kulinda mali inayosafirishwa kupitia barabara, reli, anga, au bahari dhidi ya hatari kama ajali, wizi, na uharibifu wakati wa usafirishaji.

Bima ya Biashara

Kwa wafanyabiashara, bima hii inalinda biashara yako dhidi ya hasara inayoweza kusababishwa na majanga kama moto, wizi, uharibifu wa mali, na majanga mengineyo.

Bima ya Ajali za Kazini

Kwa waajiri, bima hii inalinda wafanyakazi dhidi ya madhara yanayotokea kazini, ikiwemo ajali, ulemavu, au kifo. Hii inasaidia waajiri kutimiza wajibu wao wa kisheria kwa wafanyakazi wao.

Bima ya Safari (Travel Insurance)

Hutoa ulinzi kwa wasafiri dhidi ya hatari kama kufutwa kwa safari, upotevu wa mizigo, kuchelewa kwa safari, na dharura za kiafya wanapokuwa safarini.

WADAU WETU

Translate »