TANGAZO LA UCHAGUZI WA WAWAKILISHI WA WANACHAMA WA BANDARINI SACCOS LTD
Uongozi wa Bandarini SACCOS unapenda kuwatangazia wanachama wenye sifa za kugombea nafasi ya Uwakilishi wa Wanachama wa Bandarini SACCOS LTD katika Vituo mbalimbali kuchukua fomu kuanzia tarehe 08/05/2023 hadi tarehe 15/05/2023. Fomu zitapatikana katika ofisi za Bandarini SACCOS zilizopo Mkabala na Uwanja wa Benjamin Mkapa, Temeke, Dar es Salaam kuanzia tarehe 08/05/2023 saa 2:00 Asubuhi na mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 15/05/2023 saa 10:00 alasiri kwa ajili ya hatua zaidi za usimamizi wa zoezi hilo la uchaguzi. Aidha, tarehe, muda na mahali pa Mkutano wa Uchaguzi utazingatia Ratiba ya Mikutano ya Matawi.
SIFA ZA MGOMBEA NAFASI YA UWAKILISHI WA WANACHAMA
- Awe na elimu ya angalau stashahada, stashahada ya juu au elimu ya juu
- Awe mwadilifu na mwaminifu
- Awe hajawahi kupoteza sifa za uongozi katika ngazi yoyote ya Chama cha Ushirika
- Awe na uwezo wa kuongoza
- Awe anashiriki kikamilifu katika shughuli zote za Chama bila kutetereka
- Awe hajawahi kusababisha hasara katika Chama chochote cha ushirika
- Asiwe na tabia ya kulaza na kuchepusha madeni katika taasisi zingine
- Awe amethibitishwa kazini
- Awe mwanachama kwa kipindi kisichopungua miaka 2 na kuhudhuria mikutano ya uanachama angalau kwa mwaka mmoja
- Asiwe na deni alilolipata nje ya utaratibu